14 Ninyi mlimkataa aliyekuwa Mtakatifu na Mwenye Haki mkaomba mpewe yule muuaji. 15 Hivyo mkamwua aliye chanzo cha Uzima, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Sisi ni mashahidi wa mambo haya. 16 Imani katika jina la Yesu imempa nguvu huyu mtu ambaye mnamwona na kumfahamu. Ni kwa jina la Yesu na imani inay opatikana kwake ambayo imemponya huyu mtu kabisa, kama ninyi wenyewe mnavyoona.

Read full chapter